
VITAMBULISHO VYA TAIFA KUWAFIKIA
LINDI NA MTWARA
Mkurugenzi
wa Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) , Dickson Maimu amesema kuwa zoezi
la usajili wa watu na kuwapatia vitambulisho
hivyo litaanza katika mikoa ya Lindi,Mtwara na Pwani hivi karibuni hivyo amewataka wananchi kutoa
ushirikiano ili kufanikisha zoezi hilo.
Aidha
Mkurugenzi huyo amesema kuwa baada ya kukamilisha zoezi hilo katika mikoa ya
Dar es Salaam na mikoa yote mitano ya Zanzibar sasa wanaelekea katika mikoa hiyo
.
Akizungumza
katika mkutano wa Wafanyakazi wa Mamlaka
hiyo unaoendelea jijini hapa amesema kuwa vitambulisho hivyo vitawasaidia
Watanzania kukopesheka kwa urahisi baada ya kutambulika hivyo kuinua kipato cha
mtu mmoja mmoja na taifa kwa Ujumla,pia kuwatambua wageni na wakimbizi.
Maimu
amesema kuwa serikali imetenga fedha za kutosha katika bajeti kiasi cha
shilingi bilioni 200 ambazo zitasaidia
kufanikisha zoezi hilo na kulikamilisha,tunatarajia baada ya mikoa hiyo itafuata Kilimanjaro,Arusha na
Tanga.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) ,
Dickson Maimu akiwa anaongea na waadhishi wa habari kuhusiana na zoezi lima la ugawaji wa kitambulisho cha taifa
Kwa upande
wake Mkuu wa Wilaya ya Arusha ,Nyirembe Munasa amesema kuwa licha ya
vitambulisho hivyo kuwasaidia wananchi kiuchumi vitawasaidia katika masuala ya
ulinzi na usalama ,kutatusaidia kuwatambua wachafuzi wa amani inawezekana
wanatoka nje pia kudhibiti ugaidi.
Nyirembe
ameitaka Mamlaka hiyo kuhakikisha kuwa inatoa elimu ya kutosha kwa wananchi kwa
kupitia vyombo vya habari na taasisi mbali mbali zikiwemo shule na vyuo ili
watanzania wajue umuhimu wa vitambulisho hivyo .
Naye
Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo kwa upande wa Zanzibar,Vuai Suleman alisema kuwa
tayari zoezi hilo limekamilika katika nchi hiyo yenye mikoa 5 na wilaya
10.amewataka watanzania kutoa ushirikiano na kuwa na taarifa muhimu ikiwemo
kitambulisho cha mkazi,cheti cha kuzaliwa,vyeti vya kukupigia kura ili
kufanikisha zoezi hilo la kitaifa.
0 comments