TRA KUDHIBITI KAZI ZA WASANII
Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Mamlaka ya Mapato nchini imeanzisha mfumo wa kutoa stempu
kwa kazi za wasanii ili kudhibiti unyonywaji wa kazi hizo unaofanywa na baadhi ya wasambazaji na
wazalishaji feki hivyo kuwafanya wasanii wanufaike na kazi zao pamoja na kulipa
kodi kwa serikali.
Akizungumza na Wasanii wa muziki na filamu jijini Arusha ,Afisa
elimu kwa mlipakodi TRA,Frank Mwaselela amesema kuwa mfumo huo tayari
umerasimishwa kisheria na baada ya kutoa elimu kwa wasambazaji na wasanii
hakuna kazi yeyote itakayoruhusiwa kuuzwa pasipo kuwa na stempu.
Afisa huyo amesema kuwa mfumo huo utawasaidia wasanii
kutoibiwa kazi zao na pia kazi zao kuwa
na ulinzio wa kisheria baada ya kupitia taratibu sahihi ambazo ni kuzisajili
baraza la sanaa (BASATA) Na pia kwa baraza linalohusika na haki miliki
(COSOTA).
Naye Afisa Kodi Msafiri Mbibo kutoka makao makuu ya TRA amesema
kuwa mfumo huo wa stempu umeanza mwaka jana
utasaidia kuondoa wimbi kubwa la
wizi na uharibifu wa kazi za sanaa .
“Mpango huu utasaidia kuhakikisha kuwa wasanii kuwa mikataba
inayozingatia haki za wasanii,tayari
tuimeshaanza kufanya operesheni kuwakamata wanaouza kazi zisizo na stempu na
kuharibu mashione mkoa wa Dar tutaelekea mikoani pia” Alisema Afisa huyo
Katibu wa Chama cha Wauzaji wa kazi za wasanii jijini hapa James
Male amesema kuwa jitahada zinazofanywa na TRA na Serikali ni nzuri na ameiomba
mamlaka hiyo kuzitazama kazi walizonunua miaka ya nyuma kabla ya kuanzishwa kwa
mfumo wa stempu.
Mwenyekiti wa Chama cha Wasanii mkoani Arusha ,Kassim Digega
ameipongeza mamlaka hiyo kwa kuonyesha nia ya dhati ya kulinda kazi zao ili
waweze kunufaika na kulinufaisha taifa kwa kulipa kodi.

VITAMBULISHO VYA TAIFA KUWAFIKIA
LINDI NA MTWARA
Mkurugenzi
wa Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) , Dickson Maimu amesema kuwa zoezi
la usajili wa watu na kuwapatia vitambulisho
hivyo litaanza katika mikoa ya Lindi,Mtwara na Pwani hivi karibuni hivyo amewataka wananchi kutoa
ushirikiano ili kufanikisha zoezi hilo.
Aidha
Mkurugenzi huyo amesema kuwa baada ya kukamilisha zoezi hilo katika mikoa ya
Dar es Salaam na mikoa yote mitano ya Zanzibar sasa wanaelekea katika mikoa hiyo
.
Akizungumza
katika mkutano wa Wafanyakazi wa Mamlaka
hiyo unaoendelea jijini hapa amesema kuwa vitambulisho hivyo vitawasaidia
Watanzania kukopesheka kwa urahisi baada ya kutambulika hivyo kuinua kipato cha
mtu mmoja mmoja na taifa kwa Ujumla,pia kuwatambua wageni na wakimbizi.
Maimu
amesema kuwa serikali imetenga fedha za kutosha katika bajeti kiasi cha
shilingi bilioni 200 ambazo zitasaidia
kufanikisha zoezi hilo na kulikamilisha,tunatarajia baada ya mikoa hiyo itafuata Kilimanjaro,Arusha na
Tanga.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) ,
Dickson Maimu akiwa anaongea na waadhishi wa habari kuhusiana na zoezi lima la ugawaji wa kitambulisho cha taifa
Kwa upande
wake Mkuu wa Wilaya ya Arusha ,Nyirembe Munasa amesema kuwa licha ya
vitambulisho hivyo kuwasaidia wananchi kiuchumi vitawasaidia katika masuala ya
ulinzi na usalama ,kutatusaidia kuwatambua wachafuzi wa amani inawezekana
wanatoka nje pia kudhibiti ugaidi.
Nyirembe
ameitaka Mamlaka hiyo kuhakikisha kuwa inatoa elimu ya kutosha kwa wananchi kwa
kupitia vyombo vya habari na taasisi mbali mbali zikiwemo shule na vyuo ili
watanzania wajue umuhimu wa vitambulisho hivyo .
Naye
Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo kwa upande wa Zanzibar,Vuai Suleman alisema kuwa
tayari zoezi hilo limekamilika katika nchi hiyo yenye mikoa 5 na wilaya
10.amewataka watanzania kutoa ushirikiano na kuwa na taarifa muhimu ikiwemo
kitambulisho cha mkazi,cheti cha kuzaliwa,vyeti vya kukupigia kura ili
kufanikisha zoezi hilo la kitaifa.
